WAKATI Ken Gold ikitarajia kucheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza, benchi la ufundi limetamba kushangaza likisema litaanza kuonyesha ubora wao dhidi ya Singida Black Stars.
Timu hiyo ya mkoani Mbeya itafungua pazia ya mashindano hayo dhidi ya Singida BS ikianzia nyumbani Uwanja wa Sokoine Agosti 18 ikiwa ni mara ya kwanza kwao kushiriki ligi hiyo.
KenGold ilipanda daraja kwa rekodi nzuri kwa kutopoteza mchezo wowote wa nyumbani kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya kwenye Championship na kutwaa ubingwa wa jumla wa ligi hiyo na sasa kazi inahamia Ligi Kuu.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Fikiri Elias alisema pamoja na ugeni katika ligi hiyo, lakini wasichukuliwe kinyonge kwani wapo fiti kupambana na yeyote watakayekutana naye na shughuli itaanza Jumamosi dhidi ya Singida BS.
Alisema jina ndilo geni lakini wapo wachezaji wenye uzoefu na uwezo wa kuamua mechi na kutamba kuwa watawaheshimu wapinzani ila siyo kuwaogopa akisema kila mechi kwao ni vita ya pointi tatu.
“Ugeni ni wa jina lakini timu ni wachezaji na wapo wenye uzoefu na uwezo wa kupambana kupata ushindi kila mechi, tumekuwa na maandalizi mazuri na kazi itaanza Jumamosi dhidi ya Singida BS,” alisema.
Elias alisema anafahamu ugumu wa ligi lakini kwa uzoefu na uwezo wake anaamini watafanya vizuri kwani wamekuwa na muda mwingi kujiandaa kwa ajili ya Ligi Kuu.
Katibu mkuu wa timu hiyo, Benson Mkocha alisema hawana hofu na mashindano hayo na ndio maana walipambana kuitafuta Ligi Kuu ili kuonyesha uwezo wao ndani na nje ya uwanja.
“Kikosi kipo imara, ushirikiano upo wa ndani na nje ya uwanja hivyo tunasubiri ligi ianze ili tuwape raha mashabiki wetu waliotusapoti tangu