WANANCHI WAPINGA UJENZI WA SHULE KWENYE ENEO LA MICHEZO – MWANAHARAKATI MZALENDO

Wananchi wa Mtaa wa Wazo, Kata ya Wazo, jijini Dar es Salaam wamepinga mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Mama Samia, wakidai kuwa eneo lililochaguliwa kwa ujenzi huo ni pekee lililokuwa likitumika kwa ajili ya michezo mbalimbali katika kata hiyo.

Wananchi hao wamesema kuwa katika Kata ya Wazo hakuna eneo lingine lolote la michezo, na wamegomea ujenzi huo kwa sababu wanahofia kupoteza sehemu pekee inayowapa fursa ya kushiriki katika michezo. Wameeleza kuwa eneo hilo ni muhimu kwa maendeleo ya afya za wananchi na pia kwa ukuaji wa vipaji vya watoto na vijana.

Wananchi wameiomba Serikali kusitisha ujenzi wa shule katika eneo hilo na badala yake kuliweka kama eneo la kudumu la michezo ili kusaidia kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kukuza vipaji miongoni mwa watoto na vijana wa mtaa huo.

 

#KonceptTvUpdates

#EastAfricaTv

Related Posts