Waachieni huru viongozi wa Chadema

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemuagiza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo kuwachia huru Viongozi wote wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Agizo hilo amelitoa katika Mkutano uliofanyika Wilayani Geita wakati akizungumza na wakazi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro ambapo amemuagiza Naibu Waziri Sillo kuwachia huru wale wote waliokuwa wameshikiriwa na Jeshi la Polisi wakiwemo Viongozi wao ili waweze kukaa na kuzungumza kwa pamoja.

 

 

Related Posts