BEKI WA KULIA WA MANCHESTER UNITED AJIUNGA WEST HAM – MWANAHARAKATI MZALENDO

Klabu ya West Ham imekamilisha usajili wa beki wa kulia, Aaron Wan-Bissaka kutoka klabu ya Manchester United kwa mkataba hadi Juni 2029.

Aaron Wan-Bissaka mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na klabu ya Manchester United Juni mwaka 2019 akitokea klabu ya Crystal Palace.

Alicheza mechi yake ya kwanza ya akiwa na jezi ya United mnamo Agosti 2019, akisaidia kikosi cha aliyekuwa kocha wa kipindi hiko, Ole Gunnar Solskjaer kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Chelsea.

Katika klabu ya United nyota huyo amecheza jumla ya mechi 190 amefunga mabao mawili na kutoa asisti 13 na ameshinda makombe mawili, Kombe la FA 2024 na Kombe la Ligi 2023.

#KonceptTvUpdatesNo alt text provided for this image

Related Posts