BMH YAKUTANA NA MABALOZI – Mzalendo

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imefanya kikao na mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika Nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Astarasia kwa lengo la huduma zake zijulikane katika nchi hizo.

Balozi. Said Shaib Mussa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambaye ameakifungua kikao hicho, amewapongeza mabalozi kwa kuridhia kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa.

“Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Chandika ni mwepesi wa kutumia fursa za mabalozi maana nami nikiwa kituoni Qatar mwaka juzi tulifanya kikao kama hiki na kilizaa matunda kwangu na mabalozi wengine waliokuwa kituoni,”alisema Balozi Mussa.

Kwa upande wake, Dkt. Alphonce Chandika, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, ameomba ushirikiano kutoka kwa mabalozi na kufahamisha huduma za BMH katika nchi za nje.

“Waheshimiwa mabalozi Hospitali ya Benjamin Mkapa imeendelea kukuwa na imeweza kuwajengea uwezo baadhi ya nchi, pia tunahitaji pia kujengewa uwezo katika maeneo mengine hususani kwa nchi zilizoendelea” Alisema Dkt. Chandika.

Related Posts