WAWEKEZAJI WA NDANI MKOANI LINDI WATAKIWA KUJISAJILI TIC ILI WATAMBILIKE

Wawekezaji wa ndani Mkoani Lindi wametakiwa kujisajili na kusajili miradi yao kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili kutambuliwa na kunufaika na faida mbalimbali kama vivutio vya kikodi na kupata misamaha ya ushuru wa forodha na kodi ya ongezeko la thamani.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga wakati akifungua semina kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa wawekezaji, wafanyabiashara na wajasiriamali Mkoani humo iliyoandaliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC).

Semina hiyo ni sehemu ya kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani inayoendelea nchini.

Ndemanga ameesema wawekezaji pindi wanapojisajili na kutambulika inasaidia Serikali kuwafahamu wawekezaji nchini na kuwasaidia katika utekelezaji wa miradi yao pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili.

Akizungumzia faida za wawekezaji kujisajili TIC Meneja wa uhamasishaji kutoka katika kituo hicho Felix John amesema ni pamoja na kuvutia mitaji, kuleta tecknologia mpya hapa nchini,kutengeneza ajira kwa vijana wanaohitimu kutoka kwenye shule na vyuo mbali mbali nchini.

Aidha, Felix ameeleza kwa kipindi cha kuanzia januari hadi julai 2024 jumla ya miradi 500 imesajiliwa na ITC na matumaini yao ni kwamba miradi hiyo ikitekelezwa kwa ufanisi itaenda kuzalisha ajira takribani 121,000.




Related Posts