PAMOJA na ushindi ilioupata Dar City wa pointi 94-60 za Mchenga Stars, lakini kivutio kilikuwa ni Jamel Marbuary aliyekosha mashabiki kutokana na danki zake kwenye mchezo wa Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) kwenye Uwanja wa Donbosco Upanga.
Mabruary alifunga pointi mbili kwa mtindo wa kudanki kwa kuruka na mpira umbali wa mita tatu kwenye goli la Mchenga na kuwafanya mashabiki kulipuka kwa shangwe.
Katika mchezo huo Dar City ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo, ilianza robo ya kwanza kwa kasi, huku ikiwatumia mafundi wao Ally Mwendi na Marbuary kutupia mipira katika maeneo ya mitupo mitatu ‘three pointi’ na kuongoza katika robo tatu, kwa pointi 26-13, 24-13, 28-15, 16-15.
Mwendi aliongoza kwa kufunga pointi 24, kati ya pointi hizo alifunga katika maeneo ya mitupo mitatu mara naneĀ akifuatiwa na Mabruary aliyefunga pointi 20, huku kwa upande wa Mchenga Star, Amin Mkosa alifunga pointi 25.