Ukraine imesema jana kuwa hivi sasa inadhibiti maeneo 74 ya makaazi katika mkoa wa Kursk nchini Urusi, na ilikuwa inaendelea kusonga mbele, kwa umbali wa kati ya kilomita moja hadi tatu katika muda wa saa 24.
Maelezo hayo ya Kyiv yanakinzana na taswira inayochorwa na Urusi, ambako Meja Jenerali Apti Alaudinov alisema vikosi vya Ukraine vimedhibitiwa, huku wizara ya ulinzi ikisema mashambulizi yametibuliwa katika vijiji umbali wa kilomita 26 hadi 28 kutoka mpakani.
Soma pia: Putin asema Ukraine itapokea jibu stahiki kuhusu uvamizi wake Kursk
Ukraine iliifanyia Urusi shambulio ka kustukiza kwa kumuaga maelfu ya wanajeshi katika mkoa wa magharibi wa Kursk wiki iliyopita, katika operesheni ambayo imeipta Ukraine mafanikio yake makubwa zaidi ya uwanja wa vita tangu mwaka 2022, baada ya miezi kadhaa ya kuzidiwa mbinu na Urusi.