Kiongozi wa timu ya kikapu ya Veterani ya Old School kutoka Nairobi, Baikwinga Kobia amesema ujio wa timu yake katika bonanza lililofanyika nchini, umetokana na uhusino mkubwa walionao na Old Gurd.
Bonaza hilo la kikapu lilifanyika katika uwanja wa timu ya Old Gurd, ikishirikisha timu za Bahari, Old Gurd, Orji na Old School.
Kobia alilimbia Mwanasposti uhusino wao ulianza tangu mwaka 2015, baada ya kuwashawishi wachezaji wenzake.
“Mkataba tuliojiwekea sisi na Old Gurd, tukija Agosti na Old Gurd inawapasa waje Nairobi Desemba,” alisema Kobia.
Akizidi kuelezea alisema endapo timu ya Old Gurd itakiuka taratibu walizoziweka Kwa kutokwenda Nairobi, amedai na wao hawatafika Dar es Salaam mwakani.
Akizungumzia kuhusu bonaza hilo, alisema wachezaji wote waliweza kuonyesha viwango vikubwa.
Katika michezo yao waliyocheza, iliweza kuifunga Orji kwa pointi 24-12, na mchezo wa pili, ikafungwa na Old Gurd kwa pointi 34-36.