SIMBA WAITWA KINONDONI ISHU YA AWESU AWESU – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Afisa Habari wa klabu ya KMC Khalid Chukuchuku amesema wao kama klabu wapo tayari kusikiliza ofa ya Simba SC kama watahitaji kumsajili kiungo wao Awesu Ali Awesu.

 

 

Chukuchuku amesema hayo baada ya KMC kushinda kesi ya kimkataba dhidi ya mchezaji wao Awesu Ali Awesu, ambaye aliondoka kwenye kikosi hicho na kujiunga na Simba SC kinyume na taratibu za usajili kwa mchezaji mwenye mkataba.

 

‘’Mpira wa miguu ni mchezo wa biashara kama watakuja mezani sisi kama klabu tukiridhia ofa yao basi hakuna sababu ya kumzuia mchezaji kwenda kujiunga na klabu ya Simba.

 

“Tutakaa tutajadili thamani ya mchezaji mkataba ambao tulikuwa tumempatia, kiasi cha pesa ambacho tulikuwa tumempatia kipindi tunampa mkataba.’’amesema  Khalid Chukuchuku.

 

 

Awesu alijiunga na Simba baada ya kulipa kiasi cha shilingi Milioni 50 ambayo ilikuwa kwenye mkataba wake na KMC.

 

 

Lakini hakuishirikisha klabu kwenye mchakoto huo kitendo ambacho ni kosa kisheria kwani bado ana mkataba wa mwaka mmoja na KMC mpaka June 30, 2024..

Related Posts