REKODI zinawekwa ili zivunjwe, lakini sio kila rekodi zimekuwa zikivunjwa kuna nyingine zimekuwa zikichukua muda mrefu na nyingine zinavunjwa haraka.
Mashabiki wa soka wamepata kushuhudia rekodi mbalimbali kwenye Ligi Kuu Bara. Ligi ambayo imekuwa ikitajwa kuwa bora barani Afrika, ikishuhudiwa wachezaji na makocha mahiri kabisa wakipita na kuacha alama.
Yanga ina rekodi yake ya kutwaa mataji mengi zaidi, aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Kocha Abdallah Kibadeni aliyefunga hat trick dhidi ya watani zao rekodi ambayo haijavunjwa hadi sasa ikiwa ni miaka 40 iliyopita.
Wakati Azam FC ilianza na rekodi ya kucheza mechi 38 za Ligi Kuu bila kupoteza ambapo Azam ilifanya hivyo kati ya Feb 23, 2013, huku Yanga wakiifikia na kuivuka rekodi hiyo.
Lakini, Ligi Kuu Bara sio ishu ya kubeba ubingwa tu. Historia inaweza kuwekwa kwenye nyanja nyingi zinaweza kuwa nzuri au mbaya.
Tukiwa tunaelekea mwanzo wa msimu mpya wa ligi msimu wa 2024/25 Mwanaspoti linakuletea baadhi ya rekodi za msimu uliopita zinazotarajiwa kuvunjwa.
Msimu ulioisha kulikuwa na vipigo vingi lakini Mtibwa Sugar iliyoshuka daraja msimu huo ndio inashikirioa rekodi ya kufungwa mabao mengi zaidi, ikifungwa na Azam FC 5-0, Singida Big Stars kabla ya kubadili jina na kuitwa Black Stars ilifungwa 5-0, Simba 4-2.
Vipigo vingine ni Yanga ikiifunga KMC, 5-0, JKT Tanzania 5-0, Singida Big Stars sasa Black Stars, 5-0, Yanga ilishinda 5-1 dhidi ya Simba, wakati huo huo Azam FC ilimfunga Kagera Sugar 5-1 hizo ni baadhi ya mechi zilizokuwa na vipigo vikubwa msimu ulioisha.
Mibwa Sugar ndio inashikiria rekodi ya kufungwa mabao mengi msimu ulioisha hadi kusababisha kushuka kwao daraja.
Timu hiyo ambayo msimu ujao itashiriki Champion Ship ilifungwa mabao 54 msimu ulioisha huku ikifunga mabao 30 tu kwenye mechi 30 za msimu mzima.
Msimu ulioisha ambao Yanga alitetea taji lake mara ya tatu mfululizo ulianza Agosti 16 kama ambavyo msimu huu unatarajia kuanza bao la kwanza la msimu ulioisha lilifungwa na Elius Maguri.
Mshambuliaji huyo alifunga bao hilo akiwa na Geita Gold kwenye mchezo dhidi ya Ihefu FC kabla ya kubadili jina na kuitwa Singida Black Stars, Agosti 16 nani kuvunja rekodi ya Maguri ambaye alifunga bao dakika ya tano ya mchezo.
Ni mechi 30 zimechezwa msimu mzima lakini kati ya hizo hat trick saba tu zimefungwa huku Aziz Ki ndio akishikiria rekosi ya kufunga mbili kati ya hizo.
Kwenye hat trick hizo saba nne zimefungwa na wachezaji tofauti ambao ni Feisal Salum ‘Fei Toto’ anaecheza Azam FC, Wazir Junior akiwa KMC alifunga moja sasa anakipiga Dodoma Jiji, Jean Baleke akiwa Simba alifunga, Kipre JR akiwa Azam FC pia alifunga moja.
MECHI MFULULIZO BILA KUPOTEZA
Achana na rekodi ya msimu ulioisha 2023/24 iliyoshinda dhidi ya wapinzani wote 15 wanaoshiriki Ligi Kuu Bara.Kagera Sugar inayonolewa na Fred Felix Minziro ndio timu pekee ambayo ilikuwa imeiwekea ngumu Yanga kutokana na mchezo wa kwanza kule Kagera kwenye Uwanja wa Kaitaba kumalizika kwa suluhu hivyo Gamondi na vijana wake ilibidi kutumia nguvu ya ziada Chamazi ili kuweka rekodi hiyo.
Rekodi nyingine ambayo Yanga imeweka ni kushinda michezo 25 mfululizo katika ligi tangu msimu uliopita, mara ya mwisho kwa Wananchi kudondosha pointi nyumbani ilikuwa Oktoba 23, 2022 na walitoka sare ya bao 1-1 dhidi wa watani zao Simba.
Kwa hesabu za msimu huu wa 2023/24, Yanga ina rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 ikiwa nyumbani kuliko timu nyingine yoyote, wameshinda mechi zao zote 15, wanaowafuatia ni Azam FC ambao katika michezo 13, wameshinda 10, sare mbili na kupoteza mara moja.
Rekodi ni pointi 0 na nafasi ya pili ilishikiliwa na Azam FC kwa tofauti ya mabao manane, ambao ni katika msimu wa 2023/24, ilipowazidi Simba na kuwapiga kikumbo kwenye nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao manane tu. Msimu ulioisha nafasi iyo iliamuliwa kwa mchezo wa mwisho.
Mabao mawili ya Azam FC yakifungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ yalitosha kuibakiza timu yake nafasi ya pili na kuishusha daraja Geita Gold huku Simba wakishika nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi 69 sawa na Azam FC utofauti ni mabao ya kufunga timu iliyoshika nafasi ya pili ilikuwa na mabao 63 huku nafasi ya tatu wakifunga 59.
Rekodi inashikiliwa na nyota wawili wa timu mbili tofauti ambao ni Mudathir Yahya ambaye aliifungia timu yake ya Yanga bao dakika ya kwanza ya mchezo timu hiyo ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KMC, wakati Sospeter Bajana kiungo wa Azam FC pia alifunga bao dakika ya kwanza ya mchezo Azam FC ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania mabao yote akifunga mwenyewe.
Mabao mengine ya mapema ni dakika ya tatu yakifungwa na Ibrahim Ajibu dhidi ya Dodoma Jiji timu yake ya zamani Coastal Union ikishinda 1-0, Feisal Salum dhidi ya Tabora United wakishinda 4-0 kiungo huyo alifunga hat trick, Yassin Mgaza aliifungia timu yake ya Dodoma Jiji ikiambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tabora United.
Rekodi ni mabao 14 na inashikiliwa na Yanga katika msimu wa 2023/24. Kuwa na safu ya ulinzi ya mastaa kama Dickson Job, Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Bakari Mwamnyeto, Joyce Lomalisa na Attohoula Yao, kocha Miguel Gamondi alitengeneza ukuta wa chuma, ambao ulikuwa haupitiki kirahisi na wapinzani na kuwafanya kwa msimu mzima waruhusu mabao 14 tu kwenye Ligi Kuu bara.
Hiyo ni rekodi ambayo iliwekwa na je ni timu gani msimu huu itaweza kuivunja kama sio wao wenyewe kutokana na kuendelea na ukuta ule ule akipungua beki mmoja na kuongeza mwingine Chadrack Boka.