Konshens aibuka na Shek It kideoni

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MSANII maarufu wa kimataifa wa Jamaika, Konshens, ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Shek It’ ukiwa kwenye audio na video.

Konshens ndiye anayeongoza nyimbo nyingi kubwa zaidi za Dancehall za wakati wote duniani, safari hii anajidhihirisha kuwa mkali wa mtindo wa Dancehall.

Kibao hicho kimetayarishwa na prodyuza mkali, Costa Rica BomboCat, ambapo Konshens anaonyesha umwamba wake katika muziki wa Afro Latin.

Akizungumzia wimbo huo, Konshens anasema: “Hii inaashiria kurudi kwa Dancehall, ni muziki ninaoupenda kuliko kawaida. Ni haki yangu sasa kuhakikisha nawafurahisha pia mashabiki zangu.”

Konshens anaimba kwa hisia, uchangamfu na kutawala jukwaa katika uwezo wa hali ya juu sana.

Anaongeza: “Nilipata beat nikiwa Kenya mwaka mmoja uliopita. Nilianzisha studio yangu kwenye simu yangu tu na kurekodi nikiwa hotelini, Nairobi – Kenya. Pamoja na kelele nyingi zilizonizunguka, niliitawalisha akili yangu kwenye kurekodi wimbo wangu huo.”
Konshens anazo nyimbo kadhaa zilizotangulia kabla ya huu, kwa uchache ni Pamoja na’Bruk Off Yuh Back’, ‘Turn Me On’ na ‘Gal a Bubble’.

Related Posts