UHUSISHWAJI WA SEKTA BINAFSI KATIKA UKUZAJI VIUMBE MAJI NI JAMBO LA MSINGI – EMELDA

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti na Mafunzo ya Uvuvi, Bi. Emelda Adam ame uhusishwaji wa sekta binafsi katika tasnia nzima ya ukuzaji viumbe maji ni jambo la msingi kwa sababu kwa sababu itaongeza mnyororo wa thamani.

Akizungumza, leo Agosti 15, 2024 mkoani Mwanza katika kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji lililoudhuliwa na nchi 18 za Afrika, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti na Mafunzo ya Uvuvi, Bi. Emelda amesema ili nchi zinyanyuke kutoka hatua moja kwenda nyingine lazima ishirikishe sekta binafsi .

“na itambulike kwa sasa, ukuzaaji viumbe maji unachangia takribani pato la taifa kwa asilimia 50 kwenda 51 ya samaki wengi ambao wanazalishwa duniani.” amesema Bi. Emelda

Aidha, Bi. Emelda alisema kwa Tanzania kwa sasa katika swala la ukuzaji viumbe maji tupo katika asilimia 10 na bado tuna nafasi ya kusogea mbele zaidi kama tutaendelea kuhusisha sekta binafsi katika swala zima la myororo wa thamani katika ufugaji viumbe maji, ikiwa pamoja na kupagikana kwa chakula cha kulishia samaki pamoja na mbegu bora za samaki.

Kwa upande wake, Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Ambakisye Simtoe amesema duniani sahivi, samaki wanaofugwa wanachangia karibia asilimia 50 ya upatikanaji samaki duniani japo kwa upande wa Tanzania bado tupo chini.

Vilevile Bw. Simtoe amesema wataalamu wamekutana hapa katika kongamano hili la ukuzaji viumbe maji ili kujadili jinsi ya kuongeza shughuli za ukuzaji viumbe maji.

“kwa upande wa Tanzania tumeangalia fursa tulizonazo kama mito na maziwa katika kufanya shughuli za ufugaji samaki kwa njia ya vizimba japo moja ya changamoto zilizoonekana ni pamoja na upatikanaji wa vyakula vya kulishia samaki na mbegu bora za samaki” amesema Bw. Siimtoe

Mratibu wa Kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji, Bw. Etienne Hinrichsen amesema hili ni kongamano la tatu, la kwanza lilifanyika Kenya, mwaka huu tumefanya hapa Tanzania na kongamano hili aliishii hapa tu, kwani mwakani mwezi juni kongamano hili litafanyika nchini Uganda.

Bw. Hinrichsen aliendelea kusema kuwa watu wengi wameshwawishika na hili kongamano, na hii italeta chachu kubwa katika nchi mbalimbali katika swala la ukuzaji viumbe maji na kuzalisha zaidi.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti na Mafunzo ya Uvuvi, na ndiye Mgeni Rasmi kwenye kuhitimisha Kongamano, Bi. Emelda Adam, akizungumza na washiriki na kuwashukuru kwa mchango wao na mawazo yako katika kufanikisha Kongamano linafikia dhima, ni katika siku ya tatu ya kuhitimisha Kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji, Agosti 15, 2024, Mwanza.

Mratibu wa Kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji, Bw. Etienne Hinrichsen, akifanya majumuisho ya mada zilizotolewa na wadau wa ukuzaji viumbe maji, ni katika Kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji, Agosti 15, 2024, Mwanza.

Mratibu wa Kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji, Bw. Etienne Hinrichsen (kulia), akimpa tunzo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji na Afisa Kiungo wa Mradi wa TRUEFISH kwa Upande wa Tanzania, Dkt. Imani Kapinga (kushoto), ya kutambua mchango wake katika kuandaa Kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji, Agosti 15, 2024, Mwanza.

Mkurugenzi wa Utafiti wa Shirika la Taifa la Utafiti wa Kilimo Kenya (NARO), Dkt. Nasser Kasozi, akielezea  umuhimu wa kuunda majukwaa ya uvumbuzi wa ufugaji wa samaki kwa njia za vizimba, ni katika siku ya tatu ya Kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji, Agosti 15, 2024, Mwanza.

Afisa Maendeleo ya Biashara – Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Furaha Sichula, akielezea shughuli zinazofanywa na TADB ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa wavuvi na wafugaji, ni katika siku ya tatu ya Kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji, Agosti 15, 2024, Mwanza.

Mkuzaji Viumbe Maji kutoka Kenya, Bi. Lilly Nyamongo, akielezea changamoto za Bank nchini Kenya kutowaamini wakulima (wazalishaji wa mazao ya Uvuvi) katika utoaji Mikopo, ni katika Kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji, ikiwa ni siku ya tatu, Agosti 15, 2024, Mwanza.

Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Afrika Mashariki la Ukuzaji Viumbe Maji, kutoka nchi 18, linaloendele kwa siku ya tatu, Agosti 15, 2024, Mwanza.

Related Posts