MWENYEKITI WAZAZI TAIFA MAGANYA AWASILI KILIMANJARO KWA ZIARA YA SIKU NNE.

NA WILLIUM PAUL, HAI.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa (MCC) Fadhili Maganya amewasili mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku nne ambapo atatembelea wilaya saba za mkoa huo kukagua miradi mbalimbali pamoja na kufanya mikutano na wananchi.

Akizungumza mara baada ya kupokelewa Kia akitokea mkoani Arusha alisema kuwa, chama kitaendelea kupokea kero za wananchi na kuzitatua ambapo katika ziara yake atapokea kero za wananchi.

Kwa upande upande, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi alisema kuwa, chama kipo salama na wanaendelea kujipanga kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.



Related Posts