Bolt yapanua shughuli zake za uendeshaji hadi mkoani Morogoro

kampuni inayoongoza kwenye huduma ya taxi mtandao nchini Tanzania leo imetangaza upanuzi wa huduma zake za uendeshaji hadi mkoani Morogoro. Hatua hii ya kimkakati imekuja baada ya uzinduzi wa Treni ya kisasa ya SGR inayotoka Dar es Salaam kwenda Morogoro, ambayo imeongeza kwa kiasi kikubwa mawasiliano na kati ya miji hiyo mikuu miwili, na hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi na usafirishaji.

Kwa uendeshaji wa SGR , Morogoro itakuwa kitovu kikuu cha usafiri na kuvutia shughuli za kibiashara na kukuza utalii nchini. Bolt imekusudia kutoa suluhu za usafiri wa kuaminika, salama na utakao wanufaisha wazawa na wageni .

Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania alisema: “Tunafuraha kubwa kufikisha huduma zetu hadi Morogoro kwenye jiji lenye umuhimu. Uzinduzi wa Reli ya Standard Gauge unaashiria njia mpya ya kuiunganisha Tanzania, na tunajivunia kushiriki katika safari hii ya kuleta mabadiliko kwa kutoa huduma zetu za uhakika na salama za usafiri kwa wakazi wa Morogoro. Pia tunatarajia kutoa fursa kwa madereva wa mkoa huo na kuchangia ajira za ndani kwa kukuza uchumi wa nchi.

Utanuzi wa huduma zetu Morogoro ni uthibitisho tosha kuwa Bolt inaongeza thamani ya wigo wa soko lake nchini na pia tayari imesajili madereva kwenye mtandao wake mjini Morogoro, na inawahimiza abiria kutumia huduma zetu kwa ofa ya punguzo la asilimia 50% kwa safari zao za kwanza.

Faida nyingine ni pamoja na kuimarishwa kwa huduma kwa upatikanaji wa usafiri kwa urahisi, usalama na uhakika kwa kuinua wafanyabiashara wa ndani na kuchangia maendeleo ya kiuchumi wa Morogoro na maeneo jirani.

Madereva wa Morogoro wanajiunga vipi na Bolt?

Iwapo ungependa kuwa dereva wa Bolt, utahitajika uwe na leseni halali ya udereva ya Tanzania, simu janja ya Android au iOS yenye GPS, na upitie programu zetu/mafunzo.

Kwa maelezo zaidi au kujiandikisha udereva, tembelea https://partners.bolt.eu/

Related Posts