Dar City, UDSM ngoma ngumu BDL

WAKATI Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) ikizidi kushika kasi katika mzunguko wa pili imeonyesha timu zinazoongoza mashindano hayo, Dar City na UDSM Outsiders zikipata upinzani mkubwa kutoka kwa timu zinazofuatia.

Upinzani huo unatokana na timu zote kupambana kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya nane bora. Mbali ya timu hizo kutafuta nafasi ya kucheza hatua hiyo, pia zina nafasi ya kuongoza ligi endapo Dar City na UDSM Outsiders zitapoteza michezo.

Dar City ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo wanaongoza kwa pointi 44 wakifuatiwa na UDSM walioshinda pointi 44, ambapo uongozi wa Dar City unatokana na mabao 1946 iliyofunga, huku UDSM ikiwa nayo 1489.

Timu zinazonyemelea nafasi mbili za juu ni Savio yenye pointi 41, Vijana ‘City Bulls’ (36), Mchenga Stars (36) na JKT (35), huku zinazofuata ni Srelio (33), ABC (32), DB Oratory (30) na Pazi (29).

Timu zinazotafuta nafasi ya kujinasua zisishuke daraja ni KIUT (28), Ukonga Kings (27), Mgulani JKT (26), Jogoo (25), Crows (25) na Chui (21). Timu tatu ndizo zilizopaswa kushuka daraja.

MKOSA ATIKISA UFUNGAJI BDL

Wakati timu zikuwa zimefikisha michezo 23 kila moja, mchezaji mkongwe wa kikapu nchini, Amin Mkosa anayeichezea Mchenga Stars anaongoza kwa kufunga pointi 398.

Nyota huyo anafuatiwa na Tryone Edward wa UDSM Outsiders aliyefunga pointi 360, huku chipukizi Stanley Mtunguja kutoka Ukonga Kings akifunga 357.

Wanaofuatia ni Jonas Mushi (JKT) 344, Fortius Ngaiza (Vijana) 336, Jamel Mabruary (Dar City) 324, Halfan Mustafa (Vijana) 323, Victor Michael (Vijana) 304 na Abdul Kakwaya (DB Oratory) pointi 303.

Kwa upande wa utoaji wa asisti, Stanley Mtunguja wa Ukonga Kings anaendelea kuongoza akifanya hivyo mara 109 akifuatiwa na Erick John (Dar City) 102, Mkosa (Mchenga) 95, Cornelius Mgaza (Savio) 91, Alinani Msongele (ABC) 90 na Evans Davies (UDSM) 82.

Wengine ni Alex Bwana (Mchenga Star) 76, Dominic Kipingu (DB Oratory) 74 na Halfan Mustafa (Vijana) 73.

Related Posts