NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
KAMPUNI ya Luminous Power Technologies imeingia makubaliano ya kimkakati na Kampuni ya Swaminath Trading ili kuleta bidhaa mbalimbali vitakavyosaidia kuleta ufumbuzi wa kudumu wa upatikanaji wa Nishati nchini Tanzania.
Swaminath Trading ni mwagizaji na msambazaji wa bidhaa bora za vifaa vya umeme jua na na vifaa vya kilimo kote Afrika Mashariki tangu mwaka 2019. Kwa pamoja wamedhamilia kuleta fumbuzi wa kudumu katika upatikanaji wa nishati kwa sasa na siku zijazo.
Akizungumzia ushirikiano huo, Makamu wa Rais, Biashara ya Kimataifa, Luminous Power Technologies Revanand Andhale amesema, “Tunafuraha kuanza safari hii na Swaminath Group kwa kushirikiana na Tandhan Group, na kujikita kwa dhati kutoa vifaa vya kuaminika na vyenye bunifu wa hali ya ju na kuwaletea watanzania suluhisho la kudumu la upatikanaji wa nishati kwa Watanzania.
Amesema kuna ongezeko la mahitaji ya umeme nchini, na wanaimani kuwa vifaa hivyo vitapokelewa vyema nchini kwani bidhaa zao zinaaminiwa na mamilion ya watumiaji na wanataka watanzania pia wanufaike kupitia utumiaji wa vifaa vyao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji, Swaminath Group, Mayur Dilesh Solaki amesema “Tunafuraha kushirikiana na Luminous kuleta bidhaa bora na za kisasa. Ushirikiano wetu na Luminous unaturuhusu kuleta vifaa vya umeme mbadala vyenye viwango vilivyothibitishwa kuwa na vya ubora wa kimataifa”.
Luminous Power Technologies ni brand inayoaminika kwa bidhaa mbalimbali zenye bunifu wa hali ya juu kama vile vifaa vya kutunzia meme (Power Backups) na vifaa vya vya solar, kwa matumizi ya nyumbani, Ofisini na viwandani, vifaa vya Luminous Power Technologies ni pamoja na inverters za Betri, Panel za umeme jua na vifaa vyake. Luminous imekuwa katika biashara kwa miaka 35 sasa.
Hivi karibuni CRISIL imeongeza kiwango cha daraja kwa Luminous Power Technologies na kufikia kiwango cha daraja AAA+. Kampuni ina vitengo 7 vya uzalishaji, zaidi ya ofisi 28 za mauzo chini India, na ipo katika nchi zaidi ya 40, wafanyikazi wetu 6000 wanahudumia zaidi mawakala (washirika) 100,000 na mamilioni ya wateja duniani kote. Kauli mbiu yetu siku zote ni “Furaha Kwa Wateja Kupitia Ubunifu Na Kushirikiana Katika Utendaji”.