WAZIRI JENISTA AKABIDHIWA OFISI NA UMMY MWALIMU – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Waziri wa Afya Jenista Mhagama amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Ummy Mwalimu.

 

 

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Agosti 16, 2024 katika Ofisi za Wizara ya Afya iliyopo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ambapo Waziri Jenista amempongeza Ummy Mwalimu kwa uongozi wake ndani ya Wizara ya afya kwa kipindi chote alichofanya kazi ndani ya Sekta hiyo.

 

 

“Nakupongeza Mheshimiwa Ummy Mwalimu, hakika maendeleo haya ya Sekta ya Afya una mchango mkubwa katika kuifikisha Sekta ya Afya hapa ilipo, tutaendelea kushirkiana na kupeana ushauri zaidi katika kazi”, amesema Waziri Mhagama.

 

 

Kwa upande wake Ummy Mwalimu amempongeza Waziri Jenista kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Rais kuwa Waziri wa Afya.

 

 

“Umekuwa Kiongozi mwenye uzoefu wa kutosha ndani ya Serikali naamini kwa uwezo wako ulionao pamoja na timu hii ya Wizara unaweza kuendelea zaidi katika kuboresha Sekta ya Afya nchini”, amesema Ummy Mwalimu.

 

 

 

Related Posts