SAME.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa kupitia chama cha Mapinduzi (MCC) Fadhili Maganya amesema kuwa wataendelea kutekeleza agizo la chama la kuyalinda majimbo yote kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Maganya ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa wanachama wa ccm Tarafa ya Ndungu Jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro ambapo amesema kuwa kwa kazi kubwa alizofanya Mbunge Anne Kilango Mallecel chama kitamlinda yeye pamoja na jimbo lake.
“Wajumbe wa halmashauri kuu tulipewa kazi ya kuhakikisha tunayalinda majimbo yote lakini kwa jimbo la Same mashariki hili tayari Mbunge umeturahisishia maana wewe mwenyewe tayari umeshalilinda kazi yetu sisi ni kukuonyesha tu njia tunakuahidi tutakulinda” Amesema Maganya.