Vigogo TCD wakutana Dar kujadili uchaguzi serikali za mitaa

Dar es Salaam. Viongozi waandamizi wanaounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)  pamoja na wa Serikali wamekutaka leo Jumapili, Agosti 18, 2024 jijini Dar es Salaam.

TCD inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wamefanya kikao cha mashauriano kilichoongozwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo  madai ya 
sintofahamu ya zuio la mikutano ya hadhara kwa wapinzani.

Pia, kimejadili kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,  2024 hususani kanuni, ratiba  na miongozo ya uchaguzi.

Mbali na Mbowe ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Chadema na Jaji Mutungi, wengine walioshiriki kikao hicho Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Dorothy Semu, Kiongozi wa ACT- Wazalendo na Joseph Selasini, Makamu Mwenyekiti wa NCCR – Mageuzi, Bara.

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi na Katibu wa Oganaizesheni ya chama hicho, Issa Ussi Gavu. mawaziri, Jenista Mhagama wa Afya ambaye amemwakilisha Waziri William Lukuvi wa Sera, Bunge na Uratibu.

Pia, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamaganda Kabudi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Daniel Sillo na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk Festo Dugange.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Makatibu Wakuu John Mnyika (Chadema), Ado Shaibu (ACT Wazalendo), Hamad Masoud (CUF) na Faustine Sungura (Naibu Katibu Mkuu, NCCR Mageuzi).

Related Posts