TANESCO YAFANIKIWA KUWAWEZESHA WATEJA 84% KUWEZA KUFANYA MABORESHO YA MFUMO WA LUKU.

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limefanikiwa kuwawezesha wateja asilimia 84 katika Kanda na Mikoa ambayo walianza kufanya maboresho ya mfumo wa mita za Luku ambalo kwa Kanda ya Kati na Kaskazini zoezi hilo linatarajiwa kuanza tarehe 26,Agost 2024.

Hayo ameyaeleza Bi Irene Gowelle ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma TANESCO, Leo hii Agost 19,2024 Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu zoezi la maboresho ya mfumo wa Luku ambalo litaanza rasmi Agost 26,2024 katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida,Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga. Huku akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo la Umeme Mhandisi Kisima Nyamhanga.

Na kuongeza kuwa maboresho haya yanalenga kuenda na viwango vya mifumo ya LUKU vya Kimataifa kwa kuongeza ufani na usalama wa mita za Luku Nchini.

“Nikianza kwa upande wa mafanikio kwa kanda na mikoa ambayo zoezi lilikuwa limeshaanza ,tumefanikiwa kuwawezesha wateja asilimia 84 kuweza kufanya maboresho ya mfumo wa Luku, kwahiyo mnaweza kuona hizi asilimia zilibaki ni za mikoa ambayo tulikuwa hatujaingia, na hii imetokana na muitikio mzuri wa wateja kwa matangazo tuliyokuwa tunayatoa na wao kuyafuatulia vizuri kulipelekea kurahisha zoezi hili”.

“Zoezi hilo litaanza kufanyika katika mikoa hiyo Kuanzia tarehe 26 Agosti 2024. Maboresho haya yanalenga kuendana na viwango vya mifumo ya Luku vya kimataifa na kuongeza ufanisi na usalama wa mita za luku nchini”.

Aidha Bi Irene amesema kuwa mteja atakaponunua umeme kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe tajwa atapokea tarakimu kwenye makundi matatu ambapo kila kundi litakuwa na tarakimu ishirini ambapo kundi la kwanza na la pili la tarakimu litakuwa kwaajili ya maboresho na kundi la tatu la tarakimu litakuwa ni la umeme ulionunuliwa. Hivyo mteja aingize tarakimu za kila kundi kwa kufuata mpangilio unaosomeka kwenye risiti yake ya malipo.

“Mteja atakaponunua umeme kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe tajwa atapokea tarakimu kwenye makundi matatu,kila kundi likiwa na tarakimu ishirini. Kundi la kwanza na la pili la tarakimu yatakuwa kwaajili ya maboresho na kundi la tatu la tarakimu litakuwa ni la umeme ulionunuliwa”.

“Mteja ataingiza tarakimu za kila kundi kwa kufuata mpangilio unaosomeka kwenye risiti ya malipo au ujumbe mfupi wa simu,na kila atakapoingiza kundi moja mteja atapaswa kubonyeza alama ya kukubali ya reli au mshale wa kukubali,na hapo atakuwa amefanikiwa kuboresha mita yake na kupokea kiwango cha umeme alinunua”.

Pia gusia baadhi ya changamoto pale kinapotambukishwa kitu kipya kuwa ni uelewa mdogo kwa baadhi ya wateja kwa wengine kutokufuata zile hatua makundi katika kuingiza mita pia zipo baadhi ya mita chache ambazo zinagoma kuingiza zile change Token ambapo wamekuwa wakishauri kama mteja atapatq kadhia hiyo aweze kuwasiliana nao kwa namba za huduma kwa wateja ila wakajiridhishe na Changamoto hiyo na wakiibaini watambadilishia mteja mita pasipo gharama yeyote.

Zoezi hili la kufanya maboresho ya mita za Luku ni la bure katika maeneo yote hapa Nchini na ukomo wake itakuwa tarehe 24/11/2024.

Related Posts