Dodoma. Watu wanne wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 19, 2024 wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka mawili.
Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Kanda Dodoma na kusomewa mashtaka ya kubaka kwa kikundi (gang rape) na kumwingilia kinyume na maumbile binti ambaye hakutajwa jina lake mahakamani.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania mkoani Dodoma, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mashtaka Makao Makuu, Renatus Mkude amesema vijana hao wamekana mashtaka hayo na kutokana na unyeti wa shauri hilo wataendelea kuwa mahabusu.
Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia Mwananchi