SIKU chache tu tangu atambulishwe Mazaltan FC ya Mexico, nyota wa kimataifa wa Tanzania, Enekia Lunyamila amefunga bao kwenye mchezo wa ligi ya Sweden na kuipatia ushindi timu hiyo.
Lunyamila alitambulishwa Mazaltan akitokea Eastern Flames ya Saudia ambayo ilimaliza nafasi ya saba kati ya timu nane zinazoshiriki Ligi ya Wanawake nchini humo.
Msimu uliopita Mazaltan ambayo ni timu mpya ya Enekia ilimaliza nafasi ya 14 kati ya 18 zilizoshiriki Ligi hiyo baada ya kucheza mechi 17, ikishinda minne, sare moja na kupoteza 12.
Mchezo huo ulipiga juzi ikiwa raundi ya sita ya Ligi dhidi ya Necaxa 2-1 Uwanja wa Estadio Victoria na Enekia alifunga bao la pili lililopeleka pointi tatu kwa timu hiyo iliyoko nafasi ya 15 kati ya 18 zinazoshiriki ligi hiyo.
Bao la Enekia linaifanya timu hiyo kuipa ushindi wa kwanza tangu ligi hiyo ianze kwani kwenye mechi sita imeshinda moja na kupoteza tano.
Mchezaji huyo baada ya kujiunga na klabu hiyo ataungana na Mtanzania mwenzake, beki wa kati Julietha Singano anayekipiga Juarez iliyopo nafasi ya 11.