Makamu wa Rais, aweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Ibihwa – Bahi – MWANAHARAKATI MZALENDO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji wa Ibihwa, wilayani Bahi, mkoa wa Dodoma.

Mhe. Dkt. Mpango katika hafla hiyo ameipongeza Wizara ya Maji kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maji, ukiwemo mradi wa maji wa Ibihwa na kuongeza kasi ya uchimbaji wa visima ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama, ambapo amesisitiza ahadi ya kukamilisha mradi wa maji wa Ibihwa iwe imetekelezwa tarehe 30 Septemba, 2024.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akieleza utekelezaji wa mradi huo amewahakikishia wananchi wa kijiji cha Ibihwa kuwa, Wizara itakamilisha mradi huo mapema kabla ya tarehe 30 Septemba 2024 na kwamba huduma ya maji itafika katika mji wa Bahi.

Mradi wa Maji wa Ibihwa unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 709 na unasimamiwa na Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), utekelezaji wake ukiwa umefika asilimia 75 na umeanza kutoa huduma kwa wananchi, na utanufaisha wananchi zaidi ya elfu nane wa Kijiji cha Ibihwa.

#KonceptTvUpdates

Inaweza kuwa picha ya Watu 5, jukwaa na maandishi

Related Posts