Italia. Msako wa kuwatafuta watu sita waliokuwamo ndani ya boti ya kifahari maarufu ‘Yatch’ iliyozama kwenye Bahari ya Mediterenian karibu na eneo la Porticello nchini Italia, unaendelea asubuhi hii.
Boti hilo la kifahari lilidaiwa kuzama jana Jumatatu asubuhi Agosti 19, 2024 ambamo ndani yake kulikuwa na tajiri kutoka nchini Uingereza Mike Lynch, binti yake mwenye umri wa miaka 18 na bosi kutoka Kampuni ya Morgan Stanley.
Miongoni mwa sababu zinazotajwa kusababisha boti hilo kuzama ni dhoruba kali karibu na mji wa Palermo nchini Italia.
Boti hiyo iliyokuwa imebeba wafanyakazi 10 na abiria 12, wapo wachache walionusurika ambao waliogelea baada ya kuzama.
Vikundi vya wazamiaji wa ukozi tayari vimepata mwili wa mtu mmoja, anayedhaniwa kuwa mpishi wa ndani, na kuna hofu kwamba miili zaidi itapatikana kwenye sehemu ya boti hiyo.
Lynch ambaye aliwahi kuitwa ‘Bill Gates’ wa Uingereza amekumbwa na tatizo hilo akiwa na familia na marafiki zake wakisherehekea baada ya kuachiliwa huru kwa makosa ya ulaghai.
Mamlaka za Italia zimesema miongoni mwa waliokuwamo ndani ya boti ni Lynch, bintiye Hannah mwenye umri wa miaka 18 mwenyekiti wa benki ya Morgan Stanley International, Jonathan Bloomer na wakili wa Clifford Chance, Chris Morvillo.
Endelea kufuatilia Mwananchi.