RAIS SAMIA AZINDUA SKULI YA MAANDALIZI TASANI WAKATI WA TAMASHA LA KIZIMKAZI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amezindua Skuli ya Maandalizi Tasani katika kijiji cha Kizimkazi, Zanzibar, wakati wa Tamasha la Kizimkazi, tamasha ambalo limeendelea kujipambanua kama chachu ya maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia alieleza kuwa Tamasha la Kizimkazi limekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo, kwani limekuwa kichocheo cha utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye manufaa makubwa kwa jamii. Aliongeza kuwa mwaka huu, tamasha hili limechochea maendeleo zaidi, kwa kuwa miradi mingi imeanza kuzinduliwa na mingine inaendelea kuzinduliwa.

Rais Samia alisisitiza umuhimu wa miradi hiyo, ikiwemo Skuli ya Maandalizi Tasani, katika kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza fursa za elimu kwa watoto wa Zanzibar. Alieleza matumaini yake kuwa miradi hiyo itakuwa na athari chanya kwa maendeleo ya jamii na uchumi wa eneo hilo.

Tamasha la Kizimkazi ni mojawapo ya matukio muhimu yanayofanyika Zanzibar kila mwaka, likiwa na lengo la kuhamasisha maendeleo na utamaduni. Tamasha hilo limekuwa na mchango mkubwa katika kuzindua miradi mbalimbali ya kijamii, ikiwa ni pamoja na miradi ya elimu, afya, na miundombinu.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts