Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, Syrsky amesema kuwa hali katika mstari wa mbele wa vita imezidi kuwa mbaya na kwamba katika baadhi ya maeneo, vikosi vya Urusi vilipata ufanisi wa kimbinu na kwingineko, vikosi vya nchi yake viliweza kuboresha nafasi yake ya kimbinu.
Moscow yadai kuchukuwa udhibiti wa mji wa Novobakhmutivka
Mapema Jumapili, waziri wa ulinzi wa Urusi alidai kuwa vikosi vyake vimeuteka mji wa Novobakhmutivka katika eneo la Donetsk ulioko umbali wa kilomita 10 Kaskazini mwa mji wa Avdiivka, vilivyouteka mwezi Februari.
Tathmini kali ya hali inayowakabili wanajeshi wa Ukraine inakuja mwishoni mwa wiki ya heka heka nyingi kwa nchi hiyo.
Marekani yaidhinisha msaada kwa Ukraine
Hatimaye Marekani iliidhinisha msaada wa kifedha wa dola bilioni 61 baada ya miezi kadhaa ya mivutano ya kisiasa, kwa ununuzi wa silaha zinazohitajika na wanajeshi wa Ukrainekatika mapambano yake dhidi ya Urusi.