DEREVA WA BASI ASAKWA KWA KUSABABISHA AJALI, WATU 3 WAFARIKI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Jeshi la polisi Mkoani wa Shinyanga linamsaka dereva aliyekuwa akiendesha gari aina ya basi lenye namba za usajiri T402 EFH lililokuwa likifanya safari zake kutoka Mwanza kuelekea Dar es salaam kwa kusababisha ajali iliyopelekea vifo na majeruhi katika ajali iliyotokea hapo jana eneo la Ibadakuli manispaa ya Shinyanga.

 

 

 

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP. Janeth Magomi amesema chanjo cha ajali hiyo ni dereva huyo wa Basi kuigonga kwa nyuma gari iliyokuwa mbele lenye namba za usajili T 664 BLH lililokuwa limebeba abiria na kusababisha ajali na mara baada ya kutokea ajali hiyo alifanikiwa kukimbia na kutokomea pasipo julikana.

 

 

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi hospitali ya manispaa ya Shinyanga Dkt. Moshi Walioba ameeleza hali ya majeruhi kwa sasa na kubainisha vifo vilivyotokana na ajali hiyo.

Related Posts