DIT WAPONGEZWA KWA USIMAMIZI MZURI MRADI WA ESTRIP

Na Humphrey Shao,Michuzi Tv

Menejimenti ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) imepongezwa kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mradi wa ESTRIP unaondelea.

Pongezi hizo zimetolea na timu kutoka IUCEA ambayo imeongozwa na Dkt Joseph Cosam alipotembelea Taasisi hiyo kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Umahiri wa Tehama ambao umefadhiliwa na Benki ya Dunia.

“Tumepata fursa ya kukagua mradi kuanzia hosteli za wanafunzi mpaka jengo la madarasa ujenzi unaendelea vizuri majengo yote yamejengwa kwa kiwango cha hali ya juu hii inaonesha kuwa uongozi wa taasisi ulikuwa bega kwa bega na mkandarasi ili kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa kiwango kilichokubaliwa”amesema Dkt. Cosam

Kwa upande wake mratibu wa mradi Dkt Joseph Matiko ameeleza kuwa huu ni mradi wa kituo maalum kwa ajili ya kufundisha masuala ya teknolojia za kisasa za kidigitali na majengo hayo yatakuwa na maabara zipatazo 20 zenye kufundisha mambo ya Tehama kama usalama wa mitandao,akili mnembe pamoja na nyingine nyingi.

“Ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia themanini hivyo tutaongeza udahili wa wanafunzi lakini pia tuna uwezo wa kufundisha hata watanzania wengine kuhusu masuala ya teknolojia hii fursa kubwa sana kwa watanzania.”amesema Dkt Matiko.

Aidha ameeleza kuwa mradi huu utakapokamili utachukua wanafunzi 1800 kwa wakati mmoja.


Related Posts