FLORIDA, MAREKANI: HAIJAISHA hadi iishe. Kama ulijua wamestaafu masumbwi na kukaa tu, basi bado jaijaisha na mwaka huu utashuhudia mapambano mawili makubwa na yanayotajwa yatavutia hisia za mashabiki wengi na wadau wa mchezo huo duniani.
Ni floyd Mayweather na Mike Tyson. Wawili hawa kwa nyakati tofauti walitangaza kustaafu masumbwi na kurejea tena kwa mara nyingine na sasa wanarejea ulingoni.
Mayweather atakuwa ulingoni kule Mexico dhidi ya John Gotti III, huku Mike Tyson atakuwa ulingoni kupigana na Jake Paul Novemba mwaka huu ikiwa ni pambano la pili tangu alipotangaza kustaafu.
Tabia ya mabondia kutangaza kustaafu kisha kurejea ulingoni imekuwa ni kawaida na haijaanzia katika nyakati hizo. Hapa tumekuletea mabondia mbalimbali waliowahi kutangaza kustaafu kisha wakarejea tena ulingoni na baadhi yao walifanya vizuri na wengine waliangukia pua.
Nguli huyu wa ndondi hakuwa amepigana tangu 2011 kabla ya kutangaza kustaafu mwaka 2014.
Baada ya kukaa nje kwa muda mrefu aliamua kurejea ulingoni Septemba, 2021, kupigana na Vitor Belfort akiwa na umri wa miaka 58.
Evander alipigana na Vitor aliyekuwa na umri wa miaka 44 na alipigwa kichapo cha aibu na tangu hapo hakupanda tena ulingoni.
Mwaka 2020 alishangaza watu baada ya kurejea tena ulingoni akiwa na umri wa miaka 53 na alipigana na Roy Jones Jr ambaye pambano lao lilimalizika kwa sare.
Mike ambaye alistaafu ndondi mwaka 2005 baada ya kupigana tena na Jones Jr katika pambano hilo la raundi nane, atapanda tena ulingoni kuvaana na Jake Paul kwenye pambano ambalo litapigwa Novemba 15 mwaka huu huku Tyson akipanda akiwa na umri wa miaka 58, huku mpinzani wake akiwa na miaka 27.
Fundi huyu wa zamani wa uzito wa juu alitangaza kustaafu mwaka 2011 baada ya kupigwa na Wladimir Klitschko.
Lakini mwaka mmoja baadaye alirudi ulingoni na kupigana na Derek Chisora.
Baada ya hapo alirejea tena ulingoni mwaka 2016 alipogana mapambano manne akipoteza mawili ya mwisho dhidi ya Tony Bellew, kabla ya kutangaza kustaafu tena mwaka 2018.
Alirejea ulingoni Septemba, 2021 kupigana na rafiki yake Joe Fournier na tangu hapo hajaonekana tena ingawa mwaka 2021 hadi 2022 kulikuwa na tetesi anaweza kupigana na Tyson Fury lakini hadi sasa hakuna kilichotokea.
Kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ngumi, Hatton alipigwa mwaka 2007 na mwamba Mayweather.
Baada ya hapo alishinda mapambamo mawili kisha akaenda kupigana na Manny Pacquiao mwaka 2009 lakini akapigwa.
Akastaafu na kukaa nje ya ulingo kwa miaka mitatu kabla ya kurejea mwaka 2012 kupigana na bondia kutoka Ukraine Vyacheslav Senchenko na alipigwa.
Alirejea tena ulingoni Novemba, 2022 akiwa na umri wa miaka 43, kupigana na Marco Antonio Barrera na hakukuwa na mshindi aliyetangazwa.
Leonard ni mmoja kati ya wachezaji wa ndondi waliowahi kupendwa sana duniani, alistaafu mwaka 1984,
lakini alifanya uamuzi wa mshtuko wa kurejea miaka mitatu baadaye na kupanda uzito ili kupigana na Marvin Hagler aliyekuwa akiogopwa kwa wakati huo.
Leonard alishinda pambano lililopingwa na wadau wengi wa ngumu na baada ya hapo alipanda tena ulingoni mara tano labla ya kustaafu rasmi mwaka 1997.
Mwamba alistaafu kwa mara ya kwanza mwaka 1977 akiwa na umri wa miaka 28, lakini alirudi miaka 10 baadaye.
Alipigana mapambamo mawili na yote akapoteza kabla ya kushinda la tatu alipompiga Michael Moorer akiwa na umri wa miaka 45.
Mwaka huo aliweka rekodi yakuwa bondia wa uzito wa juu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya ngumi.
Baada ya hapo alipigana tena mapambano manne kabla ya kustaafu kwa mara ya mwisho mwaka 1997 akiwa na miaka 48.
Mwamba huyu imekuwa ni kama kawaida yake kutangaza kustaafu na kurejea tena ulingoni.
Kwa mara ya kwanza mwaka 2007, baada ya kumpiga Oscar De La Hoya alitangaza kustaafu kabla ya kurejea mwaka huo huo kupigana na Ricky Hatton, aliyembamiza kwa KO, kisha akasema tena amestaafu.
Alipumzika mwaka mmoja kisha akarejea ulingoni mwaka 2009 kisha miaka sita baadae akasema ataachana na mchezo huo baada ya kucheza na Manny Pacquiao mwaka 2015, lakini haikuwa hivyo kwani alirudi kupigana na Conor McGregor mwaka 2017 na alisema tena amestaafu na tangu hapo hajapanda tena ulingoni ingawana Mayweather alijaribu tena kuwashawishi mashabiki kuwa ulikuwa wa mwisho kumwona.
Lakini haikuwa kweli kwani baada ya hapo alirejea ulingoni mwaka 2021 kupigana na Logan Paul kisha akacheza mapambano mengine nane na Agosti 24 mwaka huu atapigana na John Gotti III kwenye ukumbi wa Arena CDMX, Mexico City, Mexico.