Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

 

SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa wananchi ngazi ya vijiji kata na wilaya ili kudhibiti ukondefu na udumavu. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).

Mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa nchini yenye kiwango cha juu cha udumavu,ambapo kwa sasa ina asi limia 31.9 kiwango kikubwa kuliko cha kitaifa cha asilimia 30 hivyo idara ya afya imejipanga kuongeza jiti hada zaidi kuhakikisha kiwango hicho kinashuka.

Hayo yamesemwa tarehe 17 Aprili, 2024 na Mganga Mkuu mkoani Songwe, Dk. Boniface Kasululu wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake.

Kasululu amesema kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa kidemografia wa mwaka 2022 kiwango cha udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 kimepungua kutoka 43% hadi 31.9% na kwamba kiwango hicho bado ni kikubwa ukilinganisha na kiwango cha kitaifa cha 30%.

Amesema mbali na kiwango hicho pia uzito pungufu mkoa una asilimia 18.1 wakati kiwango cha kitaifa ni asilimia 15, ukondefu mkoa una asilimia 0 kitaifa asilimia 5, upungufu wa damu kwa watoto mkoa ni asilimia 55 kitaifa asilimia 58, upungufu wa damu kwa akina mama mkoa asilimia 19.1 kitaifa asilimia 28.8.

Mganga Mkuu mkoani Songwe, Dk. Boniface Kasululu

Amesema kiwango cha unyonyeshaji maziwa ya mama mkoa una asilimia 60.7 kitaifa ni asilimia 59 ,na IFA intake for 90+ mkoa ni asilimia 14.1 kiwango cha kitaifa ni asilimia 8.1 na kuwa kupitia takwimu hizo wanaendelea kutoa elimu zaidi kuhakikisha viwango vinashuka ama kumalizika kabisa.

Ameongeza kuwa mkoa unakadiliwa kuwa na watoto 219,694 wenye umri wa chini ya miaka 5,katika takwimu hizo  jumla ya watoto 70,082 walio chini ya miaka 5 wanakadiliwa kuwa na udumavu,hali ili yowalazimu kuzidisha elimu zaidi ya lishe.

Amesema katika kukabiliana na tatizo la lishe duni,mkoa unaendelea kutekeleza afua mbalimbali za kuk abiliana na tatizo la lishe ikiwemo kusimamia utekelezaji wa mkataba wa viashiria vya lishe na mpango mkakati jumuishi wa pili wa kupunguza udumavu wa 2021/2022 hadi 2024/2026.

Akizungumza kwaniaba ya wanawake wenzake Anitha Samwel amesema elimu zaidi inahitajika juu ya watu kupangilia lishe sahihi kwani mkoa unalima mazao mengi ikiwemo zao la mahindi lakini kiwango cha udumavu bado kipo juu kutokana na kutojua namna ya kupangilia vyakula.

Related Posts