Kifo cha Issa Hayatou cha acha simanzi Afrika

Hii imekua wiki ya Huzuni huku Soka la Afrika likichukua siti ya nyuma wakati huu ambapo bara hili linaomboleza kifo cha Hayati Issa Hayatou.

Issa Hayatou atakumbukwa kwa ukaribu wake na viongozi wengine wa ngazi za juu kwenye soka barani humu ambako ujamaa urafiki,umoja na undugu ni maisha ya kawaida .

Hayatou alikua kiongozi shupavu ambaye ameleta mabadiliko makubwa kwenye mchezo pendwa wa soka huku msingi wa leo hii wa kimichezo na kiuchumi ukiwa umejengwa kwenye uongozi wake.

Watu wa Morocco kwa maana ya viongozi na wadau wa soka katika kada mbalimbali za uongozi wamejawa na simanzi baada ya kumpoteza shujaa huyu wa soka la Afrika huku wakikumbuka mazuri mengi yaliyojengwa chini ya uongozi wake wa kupigiwa mfano kama.sio kuigwa huku sifa kubwa ambayo iliwagusa wengi ikiwa kujitoa kwake kama.kiongozi wa juu lakini pia roho ya urafiki ambayo imemgusa kama.sio kumfaidisha karibu kila mdau wa soka la Afrika achilia mbali na wale waliofanya kazi kwa karibu na Hayatou.

Katika wakati huu mgumu Morocco inaungana na familia ya Hayatou,marafiki,ndugu,jamaa na umma wote wa wapenda soka barani Afrika kuomboleza kifo cha shujaa na tunatuma salamu za rambirambi kwa wote hasa walioko kwenye uongozi wa CAF na mashirikisho yote ya soka barani Afrika na dunia kwa jumla.

Tarek Bouchamaoui (Mjumbe wa Zamani wa Kamati kuu ya CAF na FIFA ambaye pia alikua mshauri wa Hayatou wakati akiwa rais wa CAF)
Garoua, 16 August 2024

Related Posts