Askari JWTZ, Magereza ‘waliotumwa na afande’ watinga mahakamani siku ya nne

Dodoma. Washtakiwa katika kesi ya ubakaji wa kundi na kumlawiti binti wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam, wakiingia katika jengo la kituo jumuishi cha haki jinai jijini Dodoma tayari kwa ajili ya kuendelea na kesi hiyo.

Washitakiwa hao katika kesi namba 23476 ya mwaka 2024 ambao walifika mahakamani leo Alhamisi Agosti 22, 2024 saa 2.30 asubuhi kwa ajili ya kuendelea, ni pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), MT 140105 Clinton Damas maarufu kama Nyundo.

Wengine kwenye kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, ni askari Magereza C1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson maarufu Machuche na Amin Lema maarufuKindamba.

Kesi hiyo ambayo inayoendeshwa  kwa siku tano mfululizo kuanzia Agosti 19, 2024 inasikilizwa na Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, Zabibu Mpangule.

Kwa mujibu wa Wakili wa utetezi, Godfrey Wasonga hadi jana mashahidi wawili walikuwa wameshakamilisha ushahidi wao,  huku leo wakitarajia kuendelea  kusikiliza mashahidi wengine watakaoletwa na upande wa Jamhuri..

Mashahidi waliotoa ushahidi ni mtaalamu wa uchunguzi wa mambo ya sayansi ya simu na vifaa vya kieletroniki kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi na daktari kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts