Serikali kuweka mazingira bora kwa Wafanyabiashara

Waziri wa viwanda na biashara Dr, Suleman Jafo amesema serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya ufanyaji biashara ikiwemo kuboresha miundombinu, usafiri na tehama kwa lengo la kurahisisha biashara na kupunguza gharama za uzalishaji wa huduma bora ili kukuza soko la ndani pamoja na nje ya nchi kama vile marekani.

Dr, Jafo ameyasema hayo leo wakati akifungua maonyesho ya maendeleo ya miradi ya biashara na uwekezaji Afrika chini ya Shirika la misaada la Marekani USAID, ambapo maonesho yalifanyika jijini Dar es Salaam.

” Serikali imepanga kuweka nguvu katika uwekezaji kwenye masoko na
kuboresha miundombinu kwa lengo la kurahisisha biashara pamoja na kupunguza gharama kwa wafanyabiashara na makampuni ya ndani na kuwavutia wale wenye makampuni kutoka nje ya nchini ” Amesema Jafo.

Hata hivyo Dr, Jafo amesema “Kuna haja ya kuendelea kukuza, kuimarisha uwezo wa uzalishaji na usambazaji ili kukidhi mahitaji ya masoko na kupanua mauzo ya nje kwa kutumia zaidi sekta ya jadi ili kujumuisha bidhaa zilizoongezwa thamani na za viwango vya juu”

Naye Meneja Rasilimali watu kutoka Shirika la misaada la Marekani USAID amesema ” USAID tumepanga kufanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya viwanda na biashara Afrika lakini tunaanza na Tanzania kwani kuna mazingira mazuri na tunaona wanaendelea kuweka vizuri pia, tuna miradi mbalimbali ambayo itawasaida wafanyabiashara wadogo na wakubwa kuwekeza na kufikia malengo yao bila ya changamoto”.

Related Posts