Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Songea SOUWASA, wametoa ufafanuzi juu ya huduma wanazozitoa kwa sasa ambapo malalamiko ya wateja wengi imekua ni kua na dhana ya kwamba mamlaka ya maji safi hufanya makadirio na sio kutoa Ankara kulingana na matumizi sahihi ya mteja
Hayo yameelezwa na Meneja biashara kutoka SOUWASA Jumanne Gayo wakati akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wateja wanaodhani kua mamlaka wanakadiria bili za maji, ambapo amesema mamlaka zinatoa Ankara kulingana na matumizi ya mteja na wameomba wakazi wa manispaa ya Songea kutoa ushirikianao kwa wasomaji mita pindi wanapofika majumbani kwao na kuwasihi wananchi kua na nidhamu ya matumizi ya maji na kulinda miundombinu ya maji kwa kutunza vyanzo vya maji kwa kutofanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.
Aliongeza kwa kutoa elimu na kutofautisha matumizi ya mwananchi wa nyumbani na matumizi ya wafanyabishara kutokana na matumizi wanayotumia ambapo kwa mtumiaji wa nyumbani unit moja ni 1730 na kwa wafanyabishara unit moja inasomwa kwa 1780
Kutokana na kuwepo kwa changamoto ya kutokua na maji angavu Mhandisi Charles Kitavile kutoka SOUWASA amesema kwa sasa mamlaka imetatua changamoto hiyo kwa kufanya marekebisho katika mtambo mkuu wa kusafishia maji na amewaasa wateja kama kutakua na changamoto ya kutopata maji angavu wasisite kuwasiliana na mamlaka kwa ajili ya kuwafata nyumbani kwao na kutatua changamoto hiyo kwa sababu kwa sasa mteja kutopata maji angavu ni tatizo la nyumba husika na si changamoto ya mamlaka ya maji SOUWASA
Eng Charles amesema SOUWASA wanakuja na mradi mkubwa wa miji 28 ambao ni mradi wa miaka mitatu utakaoenda kutatua changamoto ya ukosefu wa maji Manispaa ya songea hivyo anawaomba wananchi wawe wavumilivu kwani mpaka sasa mradi umeshaanza na ujenzi wa matenki yameshaanza kutekelezwa na mradi umeshakamilika kwa asilimia 5 ambapo utagharimu sh Bill 145.77
Nae kaimu mkuu kitengo cha uhusiano kutoka SOUWASA Paulo Mandia, amewasisitiza wananchi kutoa ushirikianao pindi wanapokuwa na changamoto yeyote kwa kuwasiliana nao kupitia simu ya bure,website au kufika ofisini moja kwa moja
Pia kwa wale wateja ambao watapata dharura nje ya muda wa ofisi kuna kitengo cha dharura ambacho kitawafikia kwa wakati popote pale walipo na kutatua changamoto hiyo huku akisisitiza wananchi kutunza vyanzo vya maji kwa kutofanya shughuli za kijamii karibu na vyanzo hivyo.