WAETHIOPIA 62 WATIWA NGUVUNI IRINGA KWA UHAMIAJI HARAMU – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

eshi la Polisi Mkoa wa Iringa limewadhibiti na kuwatia nguvuni raia wa kigeni kutoka Ethiopia wapatao 62 walio kuwa wakisafirishwa kuelekea Kyela Mkoani Mbeya majira ya saa 3 usiku wa Agosti 21, 2024 katika eneo la Sabasaba Mafinga Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

 

 

Akiongea na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACP Allan L. Bukumbi amesema raia hao walikuwa wakisafirisha kinyume cha utaratibu wa sheria za nchi kupitia gari aina ya Scania lenye namba za Usajiri T 631 CNF likiwa naTrela lenye namba za T 532 DGE mali ya Deodatus Chacky mkazi wa wa Dar es salaam likiwa limebeba mabomba ya kupitishia maji machafu kutoka Dar es Salaam kwenda wilayani Kyela mkoani Mbeya ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva Boniface Mwanjokolo (42) Mnyakyusa.

 

 

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limewakabidhi watuhumiwa hao 62 kwa Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa kushirikiana na Ofisi ya Mashitaka.

Related Posts