WATANZANIA LINDENI VIWANDA VYA NDANI

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akiwa ameambatana na ujumbe wake akiongea na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro Bw Saiba Edward alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro Agosti 23, 2024 wakati wa ziara yake Mkoani humo kujionea shughuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto walizonazo na kutafuta njia bora ya kuzitatua.

……

Watanzania wametakiwa kuvilinda viwanda vya ndani ya nchi na kupenda kununua na kitumia bidhaa zinazotengenezwa na viwanda hivyo ili kuvilinda na kuviwezesha kuendelea na uzalishaji, kuongeza ajira, pato la Taifa na kukuza uchumi kwa ujumla

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kulinda viwanda vya Serikalli kwa kufanya kazi kwa uadilifu, weledi, uzalendo na hofu ya Mungu ili kiepuka kusababisha uharibifu unaoweza kutokea kwa kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi kuvifufua na kuviendesha viwanda hivyo.

Ameyasema hayo Agosti 23, 2024 wakati wa Ziara yake Mkoani Kilimanjaro ambapo alipotembelea viwanda, kuongea na Wafanyabiara pamoja na Maafisa Biashara wa Mkoa huo kwa lengo la kujionea shughjuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto na kuona njia bora ya kuzitata kwa kushirikiana na Taasisi nyingine husika.

Aidha, Waziri Jafo akiwa mkoani humo alitembelea Kiwanda cha Kutengeneza Vinywaji baridi cha Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd, Kiwanda cha Bonite Bottlers Ltd, Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro, Kiwanda cha kutengeneza vipuri na mitambo mbalimbali cha KMTC, Eneo la uwekezaji la bustani ya wanyamapori ya Serval (Serval Wildlife) pamoja na Kiwanda cha Sukari Moshi (TPC).

Akiwa katika Eneo la uwekezaji la bustani ya wanyamapori ya Serval (Serval Wildlife) Dkt. Jafo amewahimiza Watanzania kutumia muda wao wa mapumziko kufanya utalii wa ndani  ili kukiza biashara ya utalii na kuvutia wafanyabiashara katika sekta hiyo ilo kukuza biashara

Katika hatua nyingine akiongea na Wafanyabiashara na Wamiliki wa Viwanda wa Mkoa wa Kilimanjaro, Waziri Jafo amewataka Watumishi wa Umma Mkoani humo kiwasaidia wafanyabiashara na amewaahidi kuwa atashirikiana na Taasisi nyingine za kisekta kutatua changamoto zilizopo na kwa lengo la kuendelea kuweka mazingira bora ya biashara kwa kupunguza gharama za uendeshaji ili kuvutia uwekezaji na ufanyaji biashara nchini

Vilevile Dkt Jafo amehamasisha utrkelezaji wa Mpango wa Viwanda Tqnzankq unaoelekeza kuwa kila Mkoa unapaswa kuanzisha Viwanda vikubwa 3, Viwanda vya kati 5, Viwanda vidogo 20 na Viwanda vidogo sana 30 ili kukukuza sekta ya viwanda kuongeza ajira na pato la Taifa

Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilomanjaro na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Raymod Mwangala ameahidi kiwa Mkoa wa Kilimanjaro utaendelea kufufua viwanda vya zamani visivyofanya kazi na kuanzisha vipya ili kiongeza ajira na pato la taifa mkoani humo.

 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akisalimiana na kuzungumza na Kaimu Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Raymod Mwangala kuhusu Maendeleo ya Sekta ya Viwanda na Biashara Mkoani humo mara alipowasili Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kuanza ziara ya kutembelea viwanda na kuongea na wafanyabiashara pamoja na Maafisa Biashara wa Mkoa huo Agosti 23, 2024 Mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akiwa ameambatana na ujumbe wake akiongea na Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd, Christopher Loiruk wakati akitembelea alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro Agosti 23, 2024 wakati wa ziara yake Mkoani humo kujionea shughuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto walizonazo na kutafuta njia bora ya kuzitatua.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Selemani Jafo (Mb.) akiwa na Viongozi mbalimbali wa Wizara, Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Siha akikaa na Simba Mweupe alipotembelea eneo la uwekezaji la bustani ya wanyamapori ya Serval (Serval Wildlife) kwa ajili ya kujionea shughuli za uwekezaji katika sekta ya utalii uliofanyika katika Wilaya ya Siha Agosti 23, 2024 wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akiwa ameambatana na ujumbe wake akiongea na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro Bw Saiba Edward alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro Agosti 23, 2024 wakati wa ziara yake Mkoani humo kujionea shughuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto walizonazo na kutafuta njia bora ya kuzitatua

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akiwa ameambatana na ujumbe wake akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelea viwanda mbalimbali Kiwanda cha Kutengeneza Vinywaji baridi cha Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd, Kiwanda cha Bonite Bottlers Ltd, Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro, Kiwanda cha kutengeneza vipuri na mitambo mbalimbali cha KMTC, Eneo la uwekezaji la bustani ya wanyamapori ya Serval (Serval Wildlife) pamoja na Kiwanda cha Sukari Moshi (TPC) Agosti 23, 2024 wakati wa ziara yake Mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji , kusikiliza changamoto walizonazo na kutafuta njia bora ya kuzitatua.

Related Posts