RAIS SAMIA – KIZIMKAZI SASA NI TAMASHA LA KITAIFA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tamasha la Kizimkazi limepandishwa hadhi kutoka tamasha la Kijji cha
Kizimkazi mpaka kuwa la kitaifa.

 

 

Akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Utalii wa Kasa kwenye Pango la Kasa lililopo eneo la Kizimkazi, Rais Samia amesema, watu wa Unguja Kusini lazima wakubaliane na mabadiliko hayo na kwamba wanapaswa kujiandaa kutumiafursa zinazoletwa na tamasha hilo.

 

 

Rais Samia pia amewataka wana Kizimkazi kuyatumia maeneo yao wanayoyamiliki kwa uangalifu na wasiyatoe bilautaratibu ili yaweze kuwa na manufaa kwao na vizazi vijavyo.

 

 

Kuhusiana na tatizo la umeme mdogo usiotosha kutokana na kasi ya uwekezaji unaofanywa Mkoa wa Kusini Unguja, Rais Samia amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohamed Mahamuod kusimamia upatikanaji wa kituo cha kusukuma umeme kwenye eneo hilo ili kukabiliana na tatizo hilo.

 

 

Mwisho, Rais Samia amemshukuru Mwekezaji wa Salaam Cave, Salehe Shaban Kassim kwa uwekezaji wake kwenye eneo hilo na kwamba atahakikisha kivutio hicho kinaongezwa kwenye vivutio vya utalii vya kitaifa ili watalii wengi zaidi waweze kukitembelea.

Related Posts