KULALA SANA WIKIENDI HUZUIA MAGONJWA YA MOYO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa kuhusiana na Afya ya Usingizi unapendekeza kuwa kupata usingizi muda mrefu wikendi kunaweza kuwa na manufaa zaidi dhidi ya kujikinga na magonjwa ya moyo kuliko ilivyodhaniwa hapo awali.

 

Kwa mujibu wa utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Tiba cha Nanjing( Nanjing Medical University), walichanganua data kutoka kwenye utafiti wa Shirika la Kitaifa la Afya na Lishe (NHANES) ambao ulihusisha zaidi ya watu wakubwa 3,400 wa Marekani.

 

 

 

Waligundua kwamba wale ambao walipata angalau saa ya ziada ya kulala usingizi wikendi walikuwa na hatari ndogo sana ya kupata magonjwa ya moyo na mishipa, ikiwa ni pamoja na shambulio la moyo na kiharusi, ikilinganishwa na wale ambao hawakupata muda wa ziada wa kulala usingizi.

 

Related Posts