Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia viongozi pamoja na wageni mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na kubainisha miradi ambayo Tanzania inashirikiana na Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia ambao unatoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea (IDA), kuitekeleza. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa nchi mbalimbali baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika.

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya, unalenga kuainisha vipaumbele vya nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA.

Akifafanua kuhusu miradi hiyo amesema Tanzania inashirikiana na IDA katika miradi mikubwa na ya kimkakati 25 katika sekta za uchukuzi, maendeleo ya kijamii, nishati, elimu, maji na uboreshaji wa mifumo ya kikodi.

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akifuatilia hutoba zilizokuwa zinawasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika.

“Mojawapo ya miradi ambayo nchi yetu inashirikiana na IDA kuitekeleza ni ile inayolenga kupunguza msongamano na kuboresha barabara za Jiji la Dar es Salaam ikiwemo ujenzi wa Kijazi Interchange na njia za Mabasi ya Mwendokasi inayohudumia wakazi zaidi ya 200,000 kwa siku. Miradi hii inachangia kwa kiasi kikubwa kubadili hali ya jiji la Dar es Salaam, hasa kiuchumi,” amesema Rais Samia.

Related Posts