Serikali kushusha kocha timu ya taifa ya Golf kwa wanawake

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali imepanga kuleta kocha wa kigeni kwa ajili ya kuifundisha timu ya Taifa ya Gofu ya wanawake.

 

Mhe. Ndumbaro amesema hayo Agosti 24, 2024 Jijini Dar Es Salaam wakati alkifunga Mashindano ya Kimataifa ya NCBA Golf Series ambapo amebainisha kuwa kocha huyo atagharamiwa na Serikali.

 

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita ya inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya vizuri katika medani za michezo kufuatia kufanya vizuri kwa wachezajin wa timu ya taifa ya gofu ya wanawake katika mashindano ya Kimataifa.

 

Katika mashindano ya hivi karibuni nyota wa Tanzania, Madina Idd ameibuka mshindi wa taji la mashindano ya wazi ya wanawake ya Uganda, (Uganda Ladies Open Championships) yaliyomalizika Jumamosi jioni mjini Entebbe.

 

Madina ambaye hakuanza vizuri katika mashindano hayo, alishinda akitokea nyuma na kukusanya jumla ya mikwaju 228 na kumpita Mtazanania mwenzake, Hawa Wanyeche aliyemaliza wa pili kwa mikwaju 230 na Mganda, Martha Babirye aliyepata mikwaju 232 katika nafasi ya tatu sawa na Mtanzania, Neema Olomi aliyepata idadi hiyo hiyo ya mikwaju.

 

Related Posts