“SIKU YA UTULIVU” TANZANIA YAZINDULIWA RASMI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Mke wa Aliyekuwa RAIS wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa ameshiriki hafla rasmi ya Uzinduzi wa “SIKU YA UTULIVU” Tanzania iliyofanyika Upanga, jijini Dar es Salaam

No alt text provided for this image
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Siku hiyo mchungaji Charles Mwantepele ambaye ndiye Mwanzilishi wa SIKU hiyo amesema ….”Wengi wetu tumekuwa tukiishi na kupitia changamoto nyingi ndani yake kama vile Changamoto katika Ndoa au Mahusiano, Sehemu za kazi, Migogoro binafsi ya nafsi katika kuyaendea mambo ambayo wakati mwingine hupelekea nafsi zetu kugubikwa na hofu, msongo wa mawazo, hali ambayo inapelekea kuhisi kuzorota afya ya Mwili kwa kitu kinachoendelea kukutafuna ndani hadi kukupa tafsiri ya kuona hauna umuhimu wa wewe kuendelea kuishi .
Kwahiyo SIKU YA KUTULIVU ndio inakuwa jibu pekeee la kuziponya Nafsi.” ameeleza Mchungaji Mwantepele
No alt text provided for this image
Kwa upande wake Mama Ana Mkapa amepongeza Mchungaji Mwantepele kwa kuja na wazo la namna hiyo ili kusaidia jamiii ya kitanzania kuponywa nafsi

Mchungaji Charles Mwantepele ameanzisha huduma maalum ya “SIKU YA UTULIVU” kwaajili ya kuponya nafsi kwa njia ya meditation itakayoambatana na vionjo vya Sanaa ya Muziki tulivu.

Hafla hiyo pia imehudhuliwa na Watu Mashuhuri hapa Nchini wakiongozwa na Mama Anna Mkapa, akiwemo Mke wa Waziri mkuu Mstaafu Joseph Warioba, Mama Warioba, katibu Mkuu Kiongozi Mtaafu Mhanjo, na Wageni wengine.

Huduma hiyo ameanzisha rasmi kwenye hafla iliyohusisha pia siku ya kusheherekea kumbukuzi ya siku ya kuzaliwa ya Mchungaji huyo.
“Siku ya Utulivu” imeanzishwa ili kusaidia binadamu kuondokana na msongo wa mawazo ambao umekuwa na matokeo mabaya kwa siku za usoni.

No alt text provided for this image
Hawa hapa ni sehemu ya wakishiriki wengine kwenye hafla ya Uzinduzi wa Huduma hio hadi ikafana zaidi; Mke wa Mchungaji Mwantepele, Mama Mch. Diana Mwantepele, Mc Anjella Mwakyanjala, Christian Mgana-Pianist, Sarah Mbwambo,
Neema Philipo- (Playing Violin 🎻 )
Joanita Emanuel – (Playing Violin 🎻 )
Anita Kalugira – (Singer and Trumpeter).
#KonceptTvUpdates

 

Related Posts