HASHEEM IBWE ALIA NA AZAM FC “TUMEKUWA AIBU KWA TAIFA” – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Kufuatia kutolewa kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika hatua ya mtoano kwa kufungwa mabao 2-1 kwa matokeo ya jumla na APR ya Rwanda, Afisa Habari wa Azam FC Hasheem Ibwe amekiri timu hiyo kulitia aibu Taifa, kwani ilikuwa ikitarajiwa kuibuka na ushindi.

 

 

“Tumewaangusha Mashabiki wetu ,Tumewaangusha Watanzania wote tumekuwa Aibu kwenye Taifa la watu mbele ya Team ambayo tunaiweza ,mbele ya Team ambayo tungeweza pata ushindi nyumbani na ugenini”,

 

 

“Hatujacheza vizuri hata kidogo mechi zote mbili kuna wakati lazima ukweli mchungu useme tumefedheheka mno. Timu yetu sio mbaya ina ubora wa hali ya juu lakini tumeondoshwa ugenini”. ameandika Ibwe na kuongeza kuwa

 

 

“Siombi Msamaha leo wala sitetei WE NEED CHANGES ,WE NEED TO CHANGE, Soon Mtafurahi, Azam Itacheza tena ,Azam Itafunga sana Azam Itakuwa Tishio RED BUTTON ON”.

 

 

Azam imetolewa kwenye michuano hiyo baada kukubali kipigo cha mabao 2-0 ugenini Rwanda na kutoka na ushindi wa bao 1-0 hapa nyumbani.

 

 

Timu ya Yanga pekee ndio imebakia kuwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika baada kushinda mabao 10 – 0 dhidi ya Vital’O ya Burundi kwa michezo miwili iliyochezwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi mkoani Dar es Salaam.

Related Posts