Arajiga wa 5-1 apewa tena Kariakoo Dabi

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imemtangaza Ahmed Arajiga kutoka mkoani Manyara kuwa mwamuzi wa kati wa mchezo wa Simba na Yanga utakaopigwa, Jumamosi hii .

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni, Yanga ikiwa mwenyeji.

Katika mchezo huo, Mohamed Mkono kutoka Tanga na Kassim Mpanga wa Dar es Salaam, watakuwa waamuzi wasaidizi, wakati Tatu Malogo kutoka Tanga ndiye atakuwa mwamuzi wa akiba.

Arajiga anakumbukwa kwa kuchezesha mchezo wa Kariakoo Dabi ya mzunguko wa kwanza uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 5-1.

Pia mwamuzi huyo amechezesha  mbili Yanga mechi zingine mbili zilizowakutanisha wakongwe hao, lakini ikiwa ni katika michuano ya Kombe ka FA.

Katika mara tatu ambazo Arajiga amechezesha mechi baina ya Simba na Yanga, matokeo yanaonesha kwamba, Yanga imeshinda mara mbili na moja ushindi umeenda upande wa Simba, hakuna sare.

Julai 25, 2021
Yanga 0-1 Simba (Fainali ASFC)

Mei 28, 2022
Yanga 1-0 Simba (Nusu fainali ASFC)

Novemba 5, 2023
Simba 1-5 Yanga (Ligi Kuu)

Related Posts