https://p.dw.com/p/4fJVc
Wajumbe wa Hamas wanatarajiwa kukutana na wapatanishi wa Qatar na Misri mjini Cairo,kutoa jibu lao kuhusiana na pendekezo hilo lililowasilishwa mwishoni mwa juma na Israel.
Wakati huohuo Israel imeshambulia katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza na kuua takriban Wapalestina 25 na kuwajeruhi wengine wengi kwa mujibu wa madaktari.