Ziara ya Naibu Meya Yazaa Matunda, Kituo cha Afya cha Tandale Kuongezwa Ukubwa

Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kunduchi Mheshimiwa Michael Urio amefanya ziara ya kushtukiza kwenye mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Abbas Tarimba leo Agosti 26, 2024 sambamba na kutembelea Kituo cha afya cha Tandale kwa lengo la kusikiliza na kuzitatu changamoto zilizopo kwenye kituo hicho.

Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kunduchi Mheshimiwa Michael Urio amefanya ziara katika maeneo tofauti kata ya tandale ukiwemo mradi wa ujenzi wa madarasa shule ya sekondari Tarimba na kubaini kuwa mkandarasi hayupo kazini muda mrefu kushoto kwake ni diwani wa kata ya tandale.

UDOGO wa eneo katika kituo cha afya cha Tandale ambao unasababisha kadhia katika utoaji huduma za afya kwa wananchi sasa kikombioni kuongezwa ukubwa. 

Kwa sasa kituo hicho kinakadiriwa kuhudumia wagonjwa zaidi ya 1,000 kwa siku ambapo ni watu 30,000 kwa mwezi kama anavyobainisha Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dk Wilfred Barinzigo. 

“Wagonjwa wengi hapa ni wale wanaotibiwa na kuondoka pamoja na wanaolazwa. Ufinyu uliopo hapa mfano jengo la wazazi halitoshi unasababisha usumbufu katika utoaji huduma,” amesema. 

“Wagonjwa wanafuata huduma nzuri mimi na wafanyakazi wenzangu tumejipanga kutoa huduma nzuri kuanzia lugha kwa wagonjwa, vipimo, matibabu tukisimamia hilo wagonjwa wataongezeka zaidi ya hapa,” amebainisha. 

Hayo yamebainishwa katika ziara ya Naibu Meya wa Kinondoni, Michael Urio aliyoifanya hii leo Agosti 26, 2024 kujionea hali halisi ya utolewaji huduma sambamba na changamoto zinazokikabili kituo hicho.

Katika kutatua hilo, Urio amesema mchakato uliopo ni kufufua mazungumzo ya kumuhamisha mmoja ya mkazi wa jirani ya eneo hilo ili kuanza upanuzi wa kituo hicho. 

“Nitazungumza na Mstahiki Meya na Mkurugenzi kwaajili ya kuongeza ukubwa wa kituo kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa wakazi wa Tandale na wale wanaotoka maeneo mengine,” amesema. 

Amesema mazungumzo na mmiliki wa eneo la jirani ambaye kwa sasa ni marehemu yalishafanyika ila kwa sasa kinachoendelea ni kukaa na familia yake kwa ajili ya kuwahamisha ili ujenzi uanze. 

“Mchakato huu upo karibuni kukamilika na watalipwa fedha lengo letu wananchi wapate huduma bora,” amesema Urio. 

Ameongeza kwamba kitendo cha kuchoma taka zinazozalishwa kituoni hapo hakifai kwani sehemu ya kuchomea ipo karibu na makazi ya watu wa karibu hivyo suala hilo litafutiwe njia mbadala. 

Kwa upande wake Diwani Kata ya Tandale Abdallah Chief amesema idadi ya wagonjwa ni kubwa na eneo ni dogo kiasi cha kuwafanya watoa huduma kushindwa kutumia utaalamu walionao katika kutoa huduma.

Related Posts