Serikali imesema itaendelea kununua zao la mahindi kwa wakulima mpaka pale watakapobakiza akiba yakuwatosha na familia zao huku matarajio ni hadi kufikia msimu ujao wakilimo hii nikutokana na uwepo wa fedha zakutosha kuendesha zoezi hilo nakuhakikisha wananchi wanapata malipo yao kwa wakati.
Hayo yameelezwa na wasimamizi wavituo mbalimbali vya Wakala wa hifadhi ya Chakula NFRA katika maeneo mbalimbali ya ununuzi wa zao hilo Mkoani Ruvuma huku wakiendelea kutoa wasiwasi wakulima na wafanyabishara wenye dhana ya kutopeleka mahindi kwakuhisi kunaukomo waununuzi wa zao hilo jambo ambalo serikali itahakikisha inaendesha zoezi hilo mpaka wananchi watakapobakiza akiba inayowatosha kwaajili ya matumizi ya chakula kwenye familia zao
Kadharika wametakiwa kuhakikisha wanarahisisha zoezi la uuzaji wa mahindi kwa NFRA kwakuzingatia ubora wa mahindi yao kwani katika kipindi hiki watalazimika kupeleka mahindi masafi yaliyokidhi ubora unaotakiwa ili kuepusha gharama za kuwalipa watu kuchambua upya ilikuondoa mahindi yaliyooza na Yale ambayo hayajakidhi viwango kwa kutokauka n.k.
Wakitoa maoni yao wakulima na wafanyabishara mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti katika vituo vya ununuzi wa wahindi katika maeneo ya Namabengo(NAMTUMBO), Mgazini(SONGEA VIJIJINI, Kizuka, Magagura na Kigonsera, wameipongeza serikali kwa kununua mahindi yao kwa bei elekezi jambo ambalo wamelipokea vizuri ukitofautisha na bei wanayouza mitaani ambayo ni chini ya shilingi 400, wameeleza kuwa kiasi hicho ni kidogo hivyo ombi kubwa nikuongeza magari ya usafirishaji wa mazao waliyouza kwa haraka kwani mahindi bado wanayo yakutosha.
Hadi hivi Sasa serikali inaendelea kununua mahindi kwa shilingi 700 bei ambayo imeonyeshwa kupokelewa vizuri na wakulima, ambapo katika vituo Kitano zaidi ya Tani elfu 10 zimekwisha nunuliwa huku wananchi wakieleza kuwa fedha wanapata kwa wakati na wametoa hamasa kwa wakulima wengine kuchangamkia fursa yakupeleka mazao kwenye vituo hivyo ili wanufaike na bei elekezi ya serikali.