MCHUANO mkali upande wa udakaji mipira ya rebound, kwa wanawake umeonyesha kwuapo kwa wachezaji Tumwagile Joshua kutoka DB Lioness na Taudencia Katumbi wa DB Lioness.
Tumwagile mwenye umbile kubwa anaongoza kwa udakaji wa mipira ya rebound mara 290, huku Taudencia ambaye ni raia Kenya akidaka mara 286.
Wakali hao wanafuatiwa na Irene Kapambala wa Polisi Stars aliyedaka mara 279, Amina Kaswa (Tausi Royals 216) na Jesca Mbowe (Pazi Queens 198).
Wengine ni Neema Yakobo (Vijana Queens 184), Beatrice Akyoo (Twalipo Queens 178), Bahome Msonga (Mchenga Queens 165) na Tukusubila Mwalusamba (Tausi Royals 161).
Kwa upande wa uzuiaji (block) anayeongoza ni Beatrice Akyoo wa Twalipo Queens aliyezuia mara 75 akifuatiwa na Neema Yakobo mara 58.
Wengine ni Irene Kapambala (Polisi Stars mara 51), Tumwagile Joshua (DB Troncatti 43), Tumaini Ndossi (Vijana Queens 35) na Jesca Mbowe (Pazi Queens 35).