TANZANIA KWENDA NA ODINGA UMOJA WA AFRIKA (AU) – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inamuuunga mkono Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).

Rais Samia ametoa kauli hiyo aliposhiriki uzinduzi wa kampeni ya kumnadi mgombea huyo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Nairobi.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Salva Kiir wa Sudan Kusini na Waziri Mkuu wa Burundi, Gervais Ndirakobuca.

Rais Samia amempongeza Odinga kwa kudumisha uhusiano na viongozi wa Afrika na wabia wake, huku akimuelezea kama kiongozi mwenye busara na mwenye uwezo wa kujenga Umoja wa Afrika.

Related Posts