Waliopata mafuriko Morogoro mjini kupatiwa mikopo

Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Morogoro ambapo walikubwa na Mafuriko na kuaribiwa makazi,biashara ,vyakula kipindi Cha mvua za masika wameanza kupatiwa mikopo na Serikali kwa kushirikiana na mamlaka zingine Ili kuwainua kiuchumi.

Joyce Mugamvi ni Afisa maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro amesema jitihada za kuhakikisha Kaya zote zilizoathirika na mafuriko kipindi cha hivi karibuni zinarudi katika Hali ya kawaida tayari ugawaji wa Mikopo kwa wafanyabiashara umeanza kwa kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali ili kuimarisha uchumi wao.

Aidha Mugamvi amesema serikali inaendelea kutoa elimu kwa wakazi waliopo maeneo hatarishi hasa namna ya kujenga nyumba zilizoimara ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi sambamba na kupatiwa elimu ya ujasiliamari itakayosaidia kujikimu kimaisha

Katika kuendelea Kuunga mkono serikali kusaidia wananchi hao Kaya 80 zilizokumbwa na mafuriko ya mvua za masika katika kata ya Lukobe halmashauri ya manispaa ya Morogoro zimepatiwa misaada mbalimbali ikiwemo chakula huku wafanyabiashara 39 wakitarajiwa kupatiwa mitaji

Akizungumza wakati akitoa misaada hiyo Beatrice Johnson ambaye ni mkurugenzi wa Taasisi ya Light for Domestic workers amesema lengo la kutoa misaada hiyo ni kuwawezesha wananchi hao ambao wamekumbwa na adha hiyo ikiwemo wanafunzi 90 ambao wamesitisha masomo yao kwa kukosa mahitaji muhimu ya shule


Awali Beatrice amesema kutokana na uhitaji wa wananchi hao bado wanahitaji misaada zaidi hasa kwa wanafunzi japo hadi sasa wamefanikiwa kugawa sare za shule, madaftari, huku wengi wao wakionyesha uhitaji zaidi
Baadhi ya wananchi waliopatiwa misaada hiyo wameshukuru taasisi hiyo sambamba na kuomba wadau wengine kujitokeza ili kutoa misaada zaidi huku wakieleza namna mafuriko hayo yalivyoathiri Mali zao

Taasisi ya Light for domestic workers ni taasisi iliyoaunganisha wadada wa kazi na kuunda chama hicho kinachotoa elimu ya ujasiriamali ikiwemo ushonaji, utengenezaji wa sabuni, na ufumaji kwa lengo la kuwainua kiuchumi.

Related Posts